Jumanne 22 Septemba 2026 - 14:32
Al-Amiri: Mkusanyiko wa Mamilioni Yemen Wafichua Uongo wa Kulengwa Makka

Hawza/ Afisa anayeshughulikia mawasiliano na mahusiano ya vyama vya kisiasa vya Yemen vinavyopinga mashambulizi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, amesisitiza kwamba utawala wa Saudi Arabia umeshindwa kwa aibu na pande zote katika nyanja zake zote za kijeshi, kisiasa na kiuchumi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Arif Al-Amiri, afisa anayeshughulikia mawasiliano na mahusiano ya vyama vya kisiasa vya Yemen vinavyopinga mashambulizi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, katika mahojiano amesisitiza kwamba; utawala wa Saudi Arabia umeshindwa kwa aibu na pande zote katika nyanja zake zote za kijeshi, kisiasa na kiuchumi. Amesema kuwa baada ya kushindwa kukabiliana na msimamo na uthabiti wa wananchi wa Yemen pamoja na vikosi vyao vya kijeshi, sasa umefikia hatua ya kuwaomba wengine waunge mkono upumbavu na majivuno yake.

Al-Amiri amesema: Adui wa Saudi Arabia anajaribu kutumia vita vya kisaikolojia na kiuelewa, akivitumia kuitawanya jamii ya Kiarabu na Kiislamu na kuigeuza mitazamo yao mbali na ukweli na uhalisia wa yale yanayoendelea leo kuhusu kushindwa kwake mfululizo, ambako kunavuruga miradi na miungano yake katika eneo hili.

Ameongeza: Kuendelea maandamano ya mamilioni ya wananchi ni uthibitisho wa wazi kwamba taifa kubwa la Yemen limeungana chini ya uongozi wake wa kimapinduzi na linaunga mkono kikamilifu chaguo na maamuzi yote ya vikosi vya kijeshi ya kuendelea kulazimisha mizania madhubuti ya kuzuia mashambulizi, na juu ya yote ikiwa ni kanuni ya “kuzingirwa uwanja wa ndege” hadi hapo mashambulizi yatakapomalizika.

Al-Amiri amebainisha: Harakati hii ya umma na mwamko unaoongezeka umefichua na kubatilisha uongo na madai ambayo Riyadh ilikuwa ikijaribu kuyasambaza kwa lengo la kuvuruga hali, kubadilisha mwelekeo wa mambo na kupotosha fikra za umma; hususan uongo wa kulengwa Makka Tukufu, ambao ulitumika kama kifuniko cha kuficha kushindwa utawala huo unaofanya mashambulizi katika medani na katika uwanja wa kisiasa.

Al-Amiri: Mkusanyiko wa Mamilioni Yemen Wafichua Uongo wa Kulengwa Makka

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha